• strict warning: Non-static method view::load() should not be called statically in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/views.module on line 879.
  • strict warning: Declaration of views_handler_filter::options_validate() should be compatible with views_handler::options_validate($form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/handlers/views_handler_filter.inc on line 589.
  • strict warning: Declaration of views_handler_filter::options_submit() should be compatible with views_handler::options_submit($form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/handlers/views_handler_filter.inc on line 589.
  • strict warning: Declaration of views_handler_filter_boolean_operator::value_validate() should be compatible with views_handler_filter::value_validate($form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/handlers/views_handler_filter_boolean_operator.inc on line 149.
  • strict warning: Declaration of views_plugin_row::options_validate() should be compatible with views_plugin::options_validate(&$form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/plugins/views_plugin_row.inc on line 135.
  • strict warning: Declaration of views_plugin_row::options_submit() should be compatible with views_plugin::options_submit(&$form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/plugins/views_plugin_row.inc on line 135.
  • strict warning: Non-static method view::load() should not be called statically in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/views.module on line 879.
  • strict warning: Non-static method view::load() should not be called statically in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/views.module on line 879.
  • strict warning: Declaration of views_plugin_style_default::options() should be compatible with views_object::options() in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/plugins/views_plugin_style_default.inc on line 25.

Edo aimaliza Mtende Super8

MSHAMBULIAJI Edward Christopher Shija leo amefunga mabao mawili wakati Simba ikiifunga Mtende ya Zanzibar kwa mabao 2-0 katika pambano la kusisimua la Kombe la Super 8 (Benki ABC) lililofanyika katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi.

Pambano hilo ni la pili kwa Simba kucheza katika michuano hiyo ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini.

Iliwachukua Simba dakika 10 tu kuandika bao la kwanza kupitia kwa Edward, ambaye alikuwa mfungaji bora wa kikosi cha pili cha Simba kabla ya kupandishwa kwenye kikosi cha wakubwa msimu uliopita.

Dakika 15 baadaye, mshambuliaji huyo ambaye sasa ni mchezaji wa timu ya taifa, alipachika bao la pili akimalizia muvu nzuri ambayo ilifanywa na wenzake.

Katika mechi hiyo, Simba ambayo inawatumia zaidi wachezaji wa kikosi cha vijana chini ya miaka 20, iliwatumia wachezaji wake Miraji Athumani, Hassan Hassan na Said Ndembla ambao wamerejea kutoka nchini Ujerumani walikowenda kucheza soka.

Simba itacheza mechi yake ya mwisho ya kundi lake mnamo Agosti 12 mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza dhidi ya timu ya Zimanimoto kutoka Zanzibar