• strict warning: Non-static method view::load() should not be called statically in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/views.module on line 879.
  • strict warning: Declaration of views_handler_filter::options_validate() should be compatible with views_handler::options_validate($form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/handlers/views_handler_filter.inc on line 589.
  • strict warning: Declaration of views_handler_filter::options_submit() should be compatible with views_handler::options_submit($form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/handlers/views_handler_filter.inc on line 589.
  • strict warning: Declaration of views_handler_filter_boolean_operator::value_validate() should be compatible with views_handler_filter::value_validate($form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/handlers/views_handler_filter_boolean_operator.inc on line 149.
  • strict warning: Declaration of views_plugin_row::options_validate() should be compatible with views_plugin::options_validate(&$form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/plugins/views_plugin_row.inc on line 135.
  • strict warning: Declaration of views_plugin_row::options_submit() should be compatible with views_plugin::options_submit(&$form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/plugins/views_plugin_row.inc on line 135.
  • strict warning: Non-static method view::load() should not be called statically in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/views.module on line 879.
  • strict warning: Non-static method view::load() should not be called statically in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/views.module on line 879.
  • strict warning: Declaration of views_plugin_style_default::options() should be compatible with views_object::options() in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/plugins/views_plugin_style_default.inc on line 25.

Simba yatoa msaada kwa Yatima

WACHEZAJI na viongozi wa klabu ya Simba leo wamehitimisha Wiki ya Simba (Simba Week) kwa kutembelea Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Maunga kilichopo Kinondoni Hananasif jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo ya aina yake ilikuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa maeneo ya jirani na kituo hicho lakini watoto ambao wametembelewa pia walionyesha furaha kubwa.

Katika tukio hilo, Simba iliwakilishwa na Makamu Mwenyekiti wake, Geofrey Nyange Kaburu aliyefuatana na wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji; Swedy Mkwabi na Said Pamba. Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Kitamba Mtawala pia alikuwemo kwenye msafara huo.

Simba imetoa zawadi ya mchele, unga, sabuni na fedha taslimu kiasi cha Sh 500,000 kwa kituo hicho na msaada huo ulipokewa na Katibu wa kituo hicho, Rashid Mpinda.

Akizungumza katika tukio hilo, Kaburu alisema Simba inafahamu kwamba ina wajibu mkubwa wa kutekeleza zaidi ya kucheza mpira pekee na ndiyo maana Wiki ya Simba iliwekwa kwa ajili ya kutekeleza wajibu wa klabu kwa washabiki wake.

"Tunafahamu pia kwamba klabu yetu ina wajibu wa kusaidia jamii pia. Hakuna sababu ya Simba kutofanya chochote kwa jamii ambayo inaisaidia kwa kuishabikia, kuingia mpirani na kununua jezi zake. Ni lazima Simba nayo ifanye kitu kwa jamii," alisema Kaburu.

Kwa upande wake, Mpinda alisema kituo hicho kilichoanzishwa mwaka 2008, kimepeta faraja kubwa kutembelewa na uongozi na wachezaji wa Simba na akatumia nafasi hiyo kuomba taasisi na makampuni binafsi kusaidia watoto wenye shida.