• strict warning: Non-static method view::load() should not be called statically in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/views.module on line 879.
  • strict warning: Declaration of views_handler_filter::options_validate() should be compatible with views_handler::options_validate($form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/handlers/views_handler_filter.inc on line 589.
  • strict warning: Declaration of views_handler_filter::options_submit() should be compatible with views_handler::options_submit($form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/handlers/views_handler_filter.inc on line 589.
  • strict warning: Declaration of views_handler_filter_boolean_operator::value_validate() should be compatible with views_handler_filter::value_validate($form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/handlers/views_handler_filter_boolean_operator.inc on line 149.
  • strict warning: Declaration of views_plugin_row::options_validate() should be compatible with views_plugin::options_validate(&$form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/plugins/views_plugin_row.inc on line 135.
  • strict warning: Declaration of views_plugin_row::options_submit() should be compatible with views_plugin::options_submit(&$form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/plugins/views_plugin_row.inc on line 135.
  • strict warning: Non-static method view::load() should not be called statically in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/views.module on line 879.
  • strict warning: Non-static method view::load() should not be called statically in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/views.module on line 879.
  • strict warning: Declaration of views_plugin_style_default::options() should be compatible with views_object::options() in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/plugins/views_plugin_style_default.inc on line 25.

Milovan: Sunzu, usihuzunike

Picha kwa Hisani ya Straikamkali.blogspot

KOCHA Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic, amemtaka mshambuliaji wake, Felix Sunzu, kutowaza sana kuhusu penalti aliyoikosa dhidi ya AS VITA na badala yake aelekeze nguvu zake katika mechi zijazo za Kombe la Kagame.

Sunzu, mshambuliaji kutoka Zambia, aliangua kilio mara baada ya pambano la hatua ya makundi dhidi ya Vita, kutokana na kukosa penalti ya dakika ya mwisho dhidi ya timu hiyo.

“Najua alihuzunika sana mara baada ya kukosa penalti lakini hicho ni kitu cha kawaida sana. Huwezi kujua mipango ya Mungu, labda kama angepata tungecheza na Atletico na labda tusingefanya vizuri. Pengine Azam ndiyo njia yetu ya ubingwa,” alisema Milovan.

Kocha huyo raia wa Serbia alisema kwa ujumla amefurahishwa na kiwango cha Sunzu kwenye michuano ya Kagame kwa vile amejituma na kujitolea kwa ajili ya timu.

“Kiujumla, bado timu hii haijacheza kwenye kiwango chake. Inahitaji kufanya mazoezi zaidi lakini hatuwezi kwa sasa kwa vile tuko kwenye mashindano. Kombe la Kagame likiisha, kutakuwa na muda mrefu wa kumaliza matatizo yanayoonekana kwa sasa,” alisema.

Ligi Kuu ya Tanzania itaanza rasmi Septemba Mosi mwaka huu na Milovan ameahidi kwamba Simba itakuwa tayari kutetea ubingwa wake wakati huo.