• strict warning: Non-static method view::load() should not be called statically in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/views.module on line 879.
  • strict warning: Declaration of views_handler_filter::options_validate() should be compatible with views_handler::options_validate($form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/handlers/views_handler_filter.inc on line 589.
  • strict warning: Declaration of views_handler_filter::options_submit() should be compatible with views_handler::options_submit($form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/handlers/views_handler_filter.inc on line 589.
  • strict warning: Declaration of views_handler_filter_boolean_operator::value_validate() should be compatible with views_handler_filter::value_validate($form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/handlers/views_handler_filter_boolean_operator.inc on line 149.
  • strict warning: Declaration of views_plugin_row::options_validate() should be compatible with views_plugin::options_validate(&$form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/plugins/views_plugin_row.inc on line 135.
  • strict warning: Declaration of views_plugin_row::options_submit() should be compatible with views_plugin::options_submit(&$form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/plugins/views_plugin_row.inc on line 135.
  • strict warning: Non-static method view::load() should not be called statically in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/views.module on line 879.
  • strict warning: Non-static method view::load() should not be called statically in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/views.module on line 879.
  • strict warning: Declaration of views_plugin_style_default::options() should be compatible with views_object::options() in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/plugins/views_plugin_style_default.inc on line 25.

Simba 2 Toto African 0

SIMBA leo imeichapa Toto African ya Mwanza kwa mabao 2-0 katika pambano kali la kirafiki lililofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

Hiyo ilikuwa ni mechi ya kwanza ya kirafiki kwa Simba katika ziara yake ya mikoa ya kanda ya ziwa iliyoanza jana (Juni 22) na kumalizika keshokutwa.

Wekundu wa Msimbazi walianza pambano hilo kwa kasi na iliwachukua dakika 17 tu kuandika bao la kwanza lililowekwa kimiani na Uhuru Selemani aliyemalizia vizuri pasi ya Abdallah Juma.

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Simba ilikuwa inaongoza kwa bao hilo moja.

Katika kipindi cha pili, Simba ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Abdallah Seseme na Hassan Khatib na nafasi zao kuchukuliwa na William Lucian (Gallas) na Jonas Mkude.

Mabadiliko hayo yalizaa matunda kwani katika dakika ya 48, Simba iliandika bao la pili lililofungwa na Salim Kinje, mchezaji mpya wa Simba aliyesajiliwa kutoka AFC Leopards ya Kenya.

Kinje alifunga bao hilo akiunganisha moja kwa moja kutoka nje ya 18 pasi ya kichwa kutoka kwa Uhuru.

Katika pambano la jana, wachezaji waliosajiliwa msimu huu walikuwa ni Waziri Hamad, Paulo Ngalema, Kiggi Makassy, Kinje na  Abdallah Juma.

Wachezaji wawili wa kikosi cha vijana Simba maarufu kwa jina la U-20, Haruna Chanonga na Lucian pia walicheza mechi yao ya kwanza kwa kikosi cha wakubwa leo hii.

Juni 24 Simba itaingia kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga kupambana na mabingwa wa soka wa Uganda, Express FC.

SIMBA; Waziri, Hassan (Gallas), Ngalema (Omar Waziri), Obadia Mungusa, Haruna Shamte, Amri Kiemba (Edward Christopher), Chanonga, Seseme (Kiggi), Abdallah (Ramadhani Salum), Kinje na Uhuru